Kuhusu sisi

Ni nia ya ushirika wa marafiki wa Ifakara kusaidia:
Hospitali ya Mt. Fransisko
zilizoko Ifakara - Tanzania.

Kwa nini?

1955 Daktari wa upasuaji Karl Schöpf kutoka Zams Tyrol alianza kujenga hospitali ya kisasa katika mji mdogo wa Ifakara uliopo katika bonde la mto Kilombero, uliokuwa na jumla ya wakazi 3000 wakati huo, katika Tanganyika, koloni la zamani la kiingereza. Hii ilichukua nafasi ya hospitali ya zamani ya misheni iliyokuwa chini ya masista wa „Baldegg“ kutoka Uswiss. Tangu 1931. Hospitali mpya ya Mt. Fransisko ilifunguliwa 1960, mwaka mmoja kabla ya Tanzania kupata uhuru. Ilikuwa chini ya daktari Karl Schöpf hadi 1961 aliporejea nchini Austria. (kong’oli: Historia ya Hospitali ya Mt. Fransisko). Kuanzia hapo uhusiano wa karibu kati ya Zams na Ifakara umeendelea.

.........Historia ya hospitali

1995 Daktari Karl Schöpf alifanya jitihada tena na kuendeleza mawasiliano ya zamani na Tanzania, akitambua matatizo ya hospitali yaliyosababishwa na hali mbaya ya Tanzania kiuchumi na hivyo kurudisha nyuma viwango vya 1969. Kutokana na jitihada za kikundi kidogo cha watu waliojitolea, vyombo vingi vya usafiri vilipatikana na elimu kwa madaktari na wauguzi iligharamiwa. Baada ya safari nyingi za Ifakara, jitihada tele na matunda yenye kuonekana, hospitali ya Mt. Fransisko imekuwa kwetu kama hospitali ya Tyrol iliyoko Tanzania.

1998 Urafikiri katika ya parokia katoliki za Zams (Austria) na Ifakara (Tanzania) ulianzishwa mwaka 1998

2004 Hatimaye ushirika uliimarishwa kiasi kwamba wafadhili binafsi waliamini ilikuwa muhimu kuanzisha ushirika na kuusajili rasmi. Hivyo „Ushirika wa Marafiki wa Ifakara“ ulianzishwa. Sasa hivi ushirika wetu umepata wanachama na wafadhili katika Austria nzima, Uswiss, Ujerumani na kusini mwa Tyrol. Wanachama wake wanafanya kazi kwa kujitolea na hujilipia gharama zote wenyewe ikiwa ni pamoja na tiketi za ndege na gharama nyingine za usafiri. Kutokana na sababu hii, michango yote huingia katika miradi ya ushirika.