Mikakati yetu
Mkakati wa kupunguza tatizo sugu la upungufu wa madaktari katika hospitali ya Mt. Francis
Ushirika wetu unafadhili mafunzo ya madaktari wawili watakaofanya kazi katika hospitali ya Mt. Francis. Mkakati huu unafadhiliwa na vyanzo viwili kwa wakati mmoja,chanzo kingine ni mradi wa maendeleo wa serikali ya Austria.
Dr. Benny Ngereza yupo katika mwaka wa kwanza wa mafunzo ya uganga msaidizi. Anahudhuria mafunzo katika kituo cha mafunzo ya afya, TTCIHI (Tanzanian Training Centre for International Health, Ifakara ), kilichopo Ifakara. Mafunzo yake yatamalizika wakati wa kipindi cha vuli 2008.
Dr. Brycson Kiwelu yupo katika mwaka wa kwanza wa mafunzo ya udhamili katika vitengo cha majeraha ya mifupa au misuli.
Anahudhuria mafunzo yake huko KCMC Moshi. Mafunzo yanadumu kwa muda wa miaka 4 na ni a ghari sana, lakini muhimu sana kwa hospitali ya Mt. Francis

Dr. Benny Ngereza, Dr. Brycson Kiwelu
Mkakati wa kuboresha hali ya maabara
Vitendea kazi vya maabara vilivyo vingi vimepitwa na wakati. Kwa upande mwingine maabara inakosa kabisa vifaa muhimu sana. Tuliamua kununua vifaa vipya ndani ya mpango wa miaka mitano uliopangwa na uongozi kwaajili ya maendeleo ya hospitali.
Katika kipindi cha vuli mwaka jana, tulitoa kifaa cha kutambua idadi ya chembechembe za damu ( Sysmex KX – 21N cha kampuni ya Etcom ), chenye thamani ya Euro 13,500.
Ndani ya wiki zijazo kitakabidhiwa kifaa cha damu cha kikemikali ( Vitros DT 60II, cha kampuni ya kiswiss (Swiss Lab. System Company), chenye kugharimu kiasi cha Euro 10,500.
Wafanyakazi wamefundishwa kwa umakini zaidi jinsi ya kutumia vifaa hivi.
Kitakachofuatia ni darubini ambazo zingehitajika sana.

Maabara katika hospitali ya Mt. Fransis

Wataalamu wa upimaji wakisubiri matokeo va vipimo vya UKIMWI
Mkakati wa kuboresha hali ya chumba cha X-ray
Kwa sasa hivi picha za x-ray zinazalishwa kwa njia ya mikono. Kazi hii si tu ni ngumu na yenye kuchukua muda mwingi, bali pia humuumiza anayefanya kazi hiyo kwani huzalishwa kemikali zenye madhara kwenye ngozi. Aidha kiwango cha ubora wa picha ni cha chini.
Atti Pahl ameagiza mtambo wa Agfa wa kusafisha picha unaojiendesha wenyewe. Kifaa hiki kimetumika tayari, lakini kimefanyiwa uchunguzi na ukarabati wa hali ya juu na hivyo kwa hakika bado kinaweza kufanya kazi kwa miaka mingi. Kifaa hiki kitakabidhiwa Ifakara hivi karibuni.

Diese antiquierten Chemietanks werden bald einer gebrauchten Entwicklungsmaschine aus Österreich weichen


