Kikumui
Tarehe 20, Mei,2007, kikundi cha sanaa maarufu kama Kikumui kiliadhimisha huko Ifakara siku ya kimataifa ya kuwakumbuka wenye virusi vya ukimwi. Hizi ni jitihada za Edgar Ikongoli na daktari Marcel Stöckle mkuu wa kitengo cha magonjwa sugu katika hospitali ya Mt. Fransisko. Kikundi hiki cha sanaa kina vijana zaidi ya 20 kutoka Ifakara, ambao mara kwa mara huvitembelea vijiji vilivyomo wilayani humo kwa kutumia usafiri wa lori. Kwa kutumia michezo yao yenye kuvutia hutoa mchango muhimu kuielimisha jamii ya bonde la mto Kilombero juu ya ugonjwa wa ukimwi.
Kwa kutumia sanaa na kwa njia yenye kufurahisha huonesha mfarakano kati ya maamuzi mbele na njia za kisasa za kujikinga na magonjwa. Mapigo ya ngoma hutumika kama msaada wa kusindikiza vielelezo kuonesha jitihada za jamii katika kupambana na gonjwa la ukimwi. Wakati huo huo vipeperushi vyenye ujumbe husambazwa. Wakati haya yanatendeka, wageni au watazamaji hupatiwa fursa ya kupima ukimwi kwa kuzingatia makubaliano binafsi.
Kikundi hiki kimepatiwa mabegi ya mgongoni yaliyotolewa na chama cha msalaba mwekundu cha Austria. Mabagi haya hubebwa na waigizaji kwa mbwembwe wakati wa maonesho.



