Hospitali teule ya Mt. Fransisko
Hospitali ya Mt.Fransisko ni mali ya jimbo katholiki la Mahenge na hutimiza jukumu lake kama hospitali teule ya wilaya kulingana na mkataba na serikali. Inawajibika kutoa huduma za afya kwa wilaya za Kilombero na Ulanga;kwa maneno mengine inahudumia jumla ya wakazi 500,000 karibu idadi sawa na jumla ya wakazi wa nchi ya Uswiss.
Ilijengwa kwa kufuata viwango vya Ulaya

Jengo la hospitali mpya lilisanifiwa.na Dr. Karl Schöpf mwenyewe. Alinuia kujenga hospitali ya kisasa yenye kiwango sawa na zile za Ulaya. Hivyo usanifu wake umezingatia hali ya hewa ya kitropiki, ina mwanga wa kutosha, uwazi na madirisha makubwa yenye kuruhusu hewa kuingia na kutoka katika pande zote. Ina veranda pana mbele ya kila wodi na katikati ya majengo kuna nafasi kubwa yenye nyasi zinazopunguzwa vizuri kila mara Kwa upande mwingine mpangilio wake wa utendaji kazi unashabihiana sana kimantiki na ule wa Ulaya.

Mlango mkuu na idara ya wagonjwa wanaofika kutibiwa na kurudi majumbani kwao

Jiko la jumuiya lilijengwa kwaajili ya wale wanaokuja kuwauguza ndugu zao
Jengo zima la hospitali limejengwa usawa wa ardhi isipokuwa majengo mawili yenye ghorofa moja yaliyounganishwa katika miisho miwili ya jengo kuu lenye veranda pana. Mmoja anaweza kwenda kwenye wodi kwa kupitia veranda hizi. Mlango wa kuingilia upo katika jengo la mbele lililojengwa usawa wa ardhi. Ofisi za utawala na ile ya mkurugenzi wa hospitali zipo katika gorofa ya kwanza. Jengo la nyuma liitwalo „Guest House“ ( Nyumba ya wageni ) hutoa huduma ya malazi kwa wageni. Misingi ya jengo zima la hospitali ni mirefu kiasi cha nusu meta zaidi ya eneo lenye nyasi zinazofyekwa vizuri mara kwa mara, hii ni kukinga jengo dhidi ya mafuriko wakati wa masika na pia wakati wa mvua zenye ngurumo kali. Mwisho, njia zote zinazounganisha majengo zimeezekwa.

Kwenye wodi kuna vyumba vikubwa kwaajili ya wagonjwa 40 na pia vyumba vidogo
Idara
Hospitali ya Mt. Fransisko ina vitanda 371, na imegawanyika katika idara za upasuaji,utaalam wa magonjwa ya ndani,magonjwa ya akina mama na uzazi, magonjwa ya watoto, magonjwa sugu na chumba cha wagonjwa mahututi. Pia kuna idara za wagonjwa wanaofika kutibiwa wakitokea majumbani kwao, wodi za kifua kikuu, tiba ya meno, tiba ya viungo vya mwili, magonjwa ya akili, ukoma, chumba cha urejeshwaji, wa afya, mazoezi na viungo bandia, idara ya x-ray na maabara. Pia maabara maalum kwaajili ya uzalishaji wa maji ya kutundikia wagonjwa, jambo ambalo Ulaya haliwezi kufikirika

Kutembelea wagonjwa katika chumba cha wagonjwa mahututi

Kwenye cha kujifungulia kuna wastani wa watoto 15 wanaozaliwa kwa siku

Wagonjwa hulazimika kukaa nje ya chumba cha opereshini kwa muda wa masaa kadhaa wakimsubiri daktari wa macho kutoka Dar-es-Salaam
Idadi ya wagonjwa ni kubwa sana
Wagonjwa wanaofika kutibiwa wakitokea majumbani kwao hufanyiwa uchunguzi na kutibiwa katika jengo maalum lililopo mbele ya hospitali, lenye idara za magonjwa ya macho, ngozi na Ukimwi ( AIDS)
Idadi ya wagonjwa inaridhisha
Jumla ya wagonjwa 100,000 hutibiwa kwa mwaka katika idara ya wagonjwa wanaotibiwa na kurejea majumbani kwao na wastani wa wagonjwa 3500 hulazwa kila mwaka. Idadi ya akina mama wazazi hufikia 5000 kwa mwaka.
Idadi hii ni kubwa ikilinganishwa na idadi ya
- madaktari bingwa 6
- madaktari 4
- na madaktari wasaidizi 8
Uongozi wa hospitali
Hospitali inaendeshwa na kamati maalum maarufu kama „Board of Governors“ Nusu ya wawakilishi ni kutoka katika jimbo la Mahenge na sehemu nyingine ni wawakilishi kutoka serikalini. Askofu Ndorobo ni mwenyekiti wa kamati.

Askofu Agapiti Ndorobo
Shughuli za kila siku huendeshwa na kamati yenye watu 3
Dr. Patience L. Kibatala, - Daktari mkuu
Fr. Cletus Uhinga - Utawala
Sr. Eustella Ngidula matroni
Fedha:
Hospitali ina ufadhili wa aina mbili; serikali ya Tanzania na Jimbo katholiki Mahenge. Gharama za uendeshaji, kama mishahara na madawa hutolewa na serikali. Ukarabati wa majengo na matumizi kama vile ununuzi wa vifaa vipya na marupurupu ya wafanyakazi hugharimiwa na Jimbo. Chanzo muhimu cha fedha ni michango ya matibabu itolewayo na wagonjwa kwaajili ya malazi, madawa na matibabu. Kiasi hiki hufanya 36% ya chanzo kizima cha pesa. Hata hivyo walio masikini kabisa hupata msamaha.
Kinadharia, mwenendo huu wa uchumi waonekana kuwa wenye mantiki; ila kwa bahati mbaya hauendani na hali halisi hata kidogo.


