Matatizo makubwa

1. Upungufu wa madaktari na hasa madaktari bingwa

Hospitali ina madaktari wasiozidi 6 Idadi hii haiwiani na idadi kubwa ya wagonjwa, hivyo mapungufu katika utoaji wa huduma ni ya lazima. Kiwango cha kuhama kwa madaktari ni cha juu sana. Sababu yaweza kuwa kwamba Ifakara ipo sehemu za ndani sana. Ni vigumu sana kumshawishi daktari kuhamia kijijini mbali sana na mji. Mishahara midogo ni tatizo jingine: Daktari msaidizi kwa mfano hupokea kiasi cha Euro 100 kwa mwezi. Mara nyingi huhitaji chanzo kingine cha fedha, mathalani ufugaji wa kuku, kilimo cha mpunga na mboga mboga ili kumudu maisha.

Wodi ya "watoto njiti"

2. Usambazaji wa madawa kutoka serikalini si wa kuaminika

Kwa kawaida hospitali hupata madawa kutoka bohari ya madawa iliyoko Dar-es-Salaam inayomilikiwa na serikali. Lakini mara nyingi madawa ama hufika kwa kuchelewa au hayapatikani kabisa. Hivyo hospitali hulazimika kununua madawa muhimu kutoka maduka binafsi ya madawa kwa bei ya juu sana.

Vifaa na vyombo mbalimbali vichakavu na vilivyoharibika

3. Hakuna bajeti inayotengwa kwaajili ya ununuzi wa vifaa vya hospitali

Hivyo vifaa vilivyo vingi vimepitwa na wakati na inaposhindikana kabisa kuvitumia haiwezekani kununua vip

4. Usambazaji wa maji na umeme si wa kuaminika

Hospitali ina visima vitatu vya kuchimbwa vinavyotoa maji kwa msaada wa pampu za maji zinazotumia umeme. Aidha, hospitali inapata umeme kutoka gridi ya Taifa. Mara nyingi umeme hukatika kwa masaa kadhaa au hata kwa siku kadhaa na hivyo kusababisha pampu za maji na vifaa vingine vinavyotumia umeme kusimama

Vifaa vya upasuaji

5. Upungufu wa vifaa vya maabara

Vifaa vingi vya maabara ni vya kiwango cha chini sana na vimepitwa na wakati. Hali hii husababisha uchunguzi wa magonjwa yaliyo mengi kuwa mgumu

Kufuatia matatizo haya, ushirika wetu umeelekeza nguvu yake katika:

1.Kufadhili elimu kwa madaktari, wataalam na kuwaendeleza wafanyakazi wengineo.
2.Kuipatia hospitali madawa na vifaa muhimu
3.Wanachama kutoka ushirika wetu huitembelea hospitali ili kusaidiana na madaktari na wauguzi na pia kuangalia vifaa.


Mikakati iliyokwishafanyika