JIOGRAFIA

Jamhuri ya muungano wa Tanzania iko Mashariki mwa Afrika, kusini mwa Kenya na ilizaliwa mwaka 1963 kutokana na Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar.

Tanzania ni Jamhuri inayoongozwa na Rais; nafasi ya juu kabisa hukaliwa na Rais ambaye huchaguliwa kila baada ya miaka mitano. Nafasi hii inakaliwa na Jakaya Kikwete kuanzia mwaka 2005.
Tanzania ni nchi yenye amani. Pamoja na wingi wa makabila iliyonao, haijapata migogoro mikubwa ya kikabila tangu ipate uhuru. Mji mkuu wa Tanzania ni Dodoma. Mji wenye wakazi wengi na mji ambao ni kitovu kiuchumi ni Dar-es-Salaam ( kwa kiarabu “Nyumba ya amani”) uliopo kando ya bahari ya Hindi. Lugha rasmi ni Kiswahili ambayo inaweza kutafsiriwa kama “Lugha ya wakazi wa pwani”, maana, kwa asili ilizungumzwa na watu wenye asili ya kiarabu, pwani ya bahari ya Hindi na kujiimarisha kama lugha ya kibiashara katika karne ya 19.

Ifakara ipo katika latitudo 8 kusini mwa ikweta katika bonde la Kilombero kusini mwa milima ya Udzungwa na ipo umbali wa kilometa 420 kusini mashariki toka Dar-es-Salaam

Kilombero ni mto uliopo kando ya mto Rufiji. Rufiji ni mto wa pili kwa ukubwa katika Afrika Mashariki. Barabara inayoelekea Ifakara katika uelekeo wa kusini magharibi, inajigawa kutoka Mikumi kwenye barabara kuu namba 1 ( iitwayo “Tanzam” ) itokayo Dar-es-Salaam kuelekea Lusaka mji mkuu wa Zambia. Baada ya barabara nzuri ya rami yenye urefu wa Km 25, inalazimu kukabiriana na barabara mbaya yenye mabonde, na yenye urefu wa takribani Km 50 hadi kufika Ifakara.. Hii hupitika kwa taabu sana wakati wa masika na wakati mwingine haipitiki kabisa. Reli ya “Tazara” iliyojengwa na shirika la msaada la kichina katika miaka ya 60 kutokea Dar-es-Salaam, inapitia Ifakara kuelekea Lusaka. Treni za abiria ni masalia yaliyotunzwa vizuri kutokea enzi za kikomunisti. Hizi hufanya safari zake mara tatu kwa juma na mara nyingi huwasili kwa kuchelewa sana. Mwisho, Ifakara pia ina kiwanja kidogo cha ndege ambapo ndege ndogo zinaweza kutua na kuruka.

Katika miaka ya hivi karibuni, idadi ya wakazi katika mji imekua kwa kasi kubwa sana, hivi sasa idadi ya wakazi inakadiriwa kuwa 100,000. Jiji linaundwa na majengo yenye gorofa moja, maarufu kama “Mainstreet” ( Mtaa maarufu ) ya tangia enzi za ukoloni kati ya miaka ya 1930 na 1939. Sambamba na mtaa huu ni mtaa wa pili kwa umaarufu ( Second mainstreet) wenye majengo yenye kiasi kidogo cha usanifu. Nyumba na vibanda visivyo katika mpangilio maalum, mimea ya kitropiki, ya kijani na yenye kuvutia, vyaonekana kutanda katika sehemu kubwa ya ya mji. Kutokana na sababu hii, ni vigumu kupata vipimo sahihi vya mji.

Hakuna kiwanda hata kimoja, ukiachia mbali kiwanda cha sukari kilichopo umbali wa Km 50, na mitambo 2 ya kuzalisha umeme iloyopo umbali wa Km 60 na Km 100. Sekta ya utalii bado ipo katika kiwango cha chini sana. Hifadhi ya wanyama ya Taifa imeanzishwa katika milima ya Udzungwa. Hii ni ndogo, lakini inapendeza sana. Kituo cha utafiti wa afya na maendeleo (tovuti www.ihi.or.tz) chenye kufanya utafiti juu ya magonjwa ya kitropiki na hasa malaria, cha Basel na kinachofanya kazi kwa kushirikiana na hospitali ya Mt. Fransisko ni cha muhimu sana kwa Ifakara.

www.ihi.or.tz

Hali ya hewa ya kitropiki, yenye majira ya mvua kuanzia mwezi Desemba hadi Mei, inatawala katika bonde la mto Kilombero. Wastani wa kiasi cha mvua kwa mwaka ni kati ya Mm 500 hadi Mm 1800. Kiasi cha joto la siku ni kati ya nyuzi 20 na 35 za sentigredi, lenye kiasi kikubwa cha unyevunyevu. Wakati wa kiangazi, kuanzia mwezi Juni hadi Augusti, hali ya hewa ni nzuri, inapendeza hata kwa Wazungu.