Madaktari kwa ajili ya Ifakara

Msaada kwa lengo la kujitegema - Mradi toka Tiroli ndani ya moyo wa Africa

Umoja wa „Madaktari kwa ajili ya Ifakara“ umeanzishwa kwa lengo la kuisaidia hospitali ya Mtakatifu Fransisi ambayo ni hospitali teule ya wilaya. Hospitali hii ambayo iko katika mji wa Ifakara, kusini mashariki mwa Tanzania, ilianzishwa na shirika la wakapuchini toka nchini Uswisi likirishikiana na Dk. Karl Schöpf ambaye kwa sasa anaishi Zams, Tiroli – Austria.

Tukishirikiana na shirika la „msaada kwa ajili ya maendeleo“ la serikali ya Austria, serikali ya mkoa wa Tiroli na watu wengi binafsi tunaelekeza jitihada zetu katika kuboresha hali ya matibabu kwa wananchi mahalia.

Wakati huo huo ni vema kufahamu kuwa sio sisi tu madaktari ndiyo tunaosaidia. Bali zipo pia taasisi nyingine nyingi na makundi mbalimbali ya wataalamu ambayo yanausaidia umoja wetu kwa jitihada kubwa: wauguzi, wana-sanaa, mafundi, watumishi wa serikali, wafanyabiashara, shule na wengine wengi.